Al-Anbiyaa 21:50
الأنبياءوَهَـٰذَا ذِكْرٌ مُّبَارَكٌ أَنزَلْنَـٰهُ ۚ أَفَأَنتُمْ لَهُۥ مُنكِرُونَ
Na haya ni makumbusho yaliyobarikiwa, tuliyoyateremsha. Basi je! Mnayakataa?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na haya ni makumbusho yaliyo barikiwa, tuliyo yateremsha. Basi je! Mnayakataa? [50]
[50] Na hii Qur'ani ni kumbusho, lenye kheri nyingi. Tumekuteremshieni kama tulivyo mteremshia Musa. Basi yawaje nyinyi muikatae, na hali nyinyi ndio mnao stahiki zaidi kuiamini kuliko watu wote!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hii Qur’ani ambayo Allah Mtukufu Ameiteremsha kwa Mtume Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, ni ukumbusho kwa anayejikumbusha nayo na akatekeleza amri Zake na akajiepusha na makatazo Yake, ina kheri nyingi na manufaa makubwa. Je, mnaikanusha na hali ina upeo wa uwazi na ufunuzi?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net