Al-Anbiyaa 21:48
الأنبياءوَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ ٱلْفُرْقَانَ وَضِيَآءً وَذِكْرًا لِّلْمُتَّقِينَ
Na kwa yakini tuliwapa Musa na Harun kipambanuzi, na mwangaza, na makumbusho kwa wacha Mungu,
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa yakini tuliwapa Musa na Haaruni kipambanuzi, na mwangaza, na makumbusho kwa wachamngu, [48]
[48] Na Musa na Haaruni tuliwapa Taurati ya kupambanua baina ya kweli na uwongo, na halali na haramu. Na juu ya hivyo hiyo ni nuru ya kuwaongoa watu wafuate njia ya kheri na uwongozi mwema, na ni kumbusho la kuwafaa wachamngu...
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika, tulimpa Mûsã na Hãrûn hoja na ushindi juu ya maadui wao na pia Kitabu, nacho ni Taurati, ambacho kwacho tumepambanua baina ya ukweli na urongo, na ambacho ni nuru ambayo kwayo wanajiongoza wachamungu wenye kuogopa adhabu ya Mola wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net