Al-Anbiyaa 21:47
الأنبياءوَنَضَعُ ٱلْمَوَٰزِينَ ٱلْقِسْطَ لِيَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْـًٔا ۖ وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا ۗ وَكَفَىٰ بِنَا حَـٰسِبِينَ
Nasi tutaweka mizani za uadilifu kwa Siku ya Kiyama. Basi nafsi haitadhulumiwa kitu chochote. Hata ikiwa ni uzito wa chembe ya khardali, tutaileta. Nasi tunatosha kuwa wenye kufanya hisabu sawasawa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nasi tutaweka mizani za uadilifu kwa Siku ya Kiyama. Basi nafsi haitadhulumiwa kitu chochote. Hata ikiwa ni uzito wa chembe ya khardali tutaileta. Nasi tunatosha kuwa washika hisabu. [47]
[47] Na Sisi tunaweka mizani ya kupimiwa kwa uadilifu Siku ya Kiyama. Basi hadhulumiwi mtu kwa kupunguziwa wema wake au kuongezewa maovu yake. Hata ikiwa ni kiasi ya uzani wa chembe ndogo hii tutaileta na tutaihisabu. Na yatosha kuwa ni Sisi ndio wa kuhisabu. Basi hapana atakaye dhulumiwa kitu. Maoni ya wataalamu juu ya Aya ya 47: "Nasi tutaweka mizani za uadilifu kwa Siku ya Kiyama. Basi nafsi haitadhulumiwa kitu chochote. Hata ikiwa ni uzito wa chembe ya khardali tutaileta. Nasi tunatosha kuwa washika hisabu.": Aya hii tukufu inaonyesha kuwa chembe ya khardali ni hadi ya udogo katika mizani. Imethibitika kwa majaribio ya sayansi kuwa Kilogram ya chembe za khardali ni chembe 913,000. Kwa hivyo chembe moja ya khardali ni takriban sehemu moja katika elfu ya gram, yaani ni takriban sawa na Miligram moja. Na huu ni uzito mdogo kabisa unao juulikana katika mbegu za mimea mpaka sasa. Kwa hivyo hutumiwa katika kupimiwa vitu vidogo vidogo kabisa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Ataiweka Mizani ya uadilifu kwa ajili ya Hesabu katika siku ya Kiyama. Hawatadhulumiwa hawa wala wengine kitu chochote, hata kama ni kitendo, kizuri au kibaya, cha kadiri ya chungu mdogo, kitazingatiwa katika hesabu ya mwenyewe. Na inatosha kuwa Allah Mtukufu ni Mwenye kuyadhibiti matendo ya waja Wake na ni Mwenye kuwalipa kwayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net