Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 45

Al-Anbiyaa 21:45

الأنبياء

قُلْ إِنَّمَآ أُنذِرُكُم بِٱلْوَحْىِ ۚ وَلَا يَسْمَعُ ٱلصُّمُّ ٱلدُّعَآءَ إِذَا مَا يُنذَرُونَ

Maana

Sema: Mimi ninawaonya kwa ufunuo (wahyi). Na viziwi hawasikii wito wanapoonywa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Mimi nakuonyeni kwa Wahyi. Na viziwi hawasikii wito wanapo onywa. [45]

[45] Ewe Nabii! Sema: Sikuhadharisheni kwa maneno yanayo tokana nami. Lakini nakuhadharisheni kwa Wahyi (Ufunuo) unao tokana na Mwenyezi Mungu Mtukufu ulio nijia mimi. Na huo ni wa Haki na kweli. Lakini hao kwa sababu ya kupuuza kwao kurefu kuipuuza Sauti ya Haki, Mwenyezi Mungu ameyaziba masikio yao mpaka wakawa kama viziwi. Na kiziwi hasikii Wito anapo hadharishwa na adhabu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia wale uliotumwa kwao, «Siwaonyi na adhabu ya Allah Mtukufu isipokuwa ni kwa wahyi wa Allah Mtukufu,» nao ni Qur’ani. «Lakini makafiri hawasikii yale wanayosomewa kusikia kwa kuzingatia wanapoonywa, na kwa hivyo hawafaidiki nayo».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net