Al-Anbiyaa 21:44
الأنبياءبَلْ مَتَّعْنَا هَـٰٓؤُلَآءِ وَءَابَآءَهُمْ حَتَّىٰ طَالَ عَلَيْهِمُ ٱلْعُمُرُ ۗ أَفَلَا يَرَوْنَ أَنَّا نَأْتِى ٱلْأَرْضَ نَنقُصُهَا مِنْ أَطْرَافِهَآ ۚ أَفَهُمُ ٱلْغَـٰلِبُونَ
Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je, hawaoni ya kwamba Sisi tunaijia ardhi tukiipunguza kutokea kwenye ncha zake? Basi je, hao ndio watashinda?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je, hawaoni ya kwamba Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza ncha zake? Basi je! Hao ni wenye kushinda? [44]
[44] Sisi hatufanyi haraka kuwaadhibu hawa kwa ukafiri wao, lakini tunawapururia na kuwastarehesha katika uhai wa dunia, kama tulivyo wastarehesha baba zao kabla yao, mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je! Wanajitia upofu hawaoni yanao wazunguka wakaona kuwa Sisi tunaiendea nchi na tukaipunguza ncha zake kwa ushindi wa Waumini? Ni wao ndio wenye kushinda au Waumini ambao Mwenyezi Mungu amewaahidi kuwasaidia na kuwaunga mkono? Maoni ya wataalamu juu ya Aya 44: "Je, hawaoni ya kwamba Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza mipaka yake? Basi je! Hao ni wenye kushinda?": Aya hii ni katika Aya za miujiza ya kisayansi katika Qur'ani Tukufu. Hii inaonyesha kuwa dunia si mduwara kaamili. Na wataalamu wa sayansi hawakutamakani kupima masafa ya dunia baraabara mpaka kiasi ya miaka 250 tu takriban, walipo ingia kikundi cha mabingwa walio khusika na ilimu ya kupima marefu baina ya daraja mbili za urefu longitudes. Na hayo kwa pahala mbali mbali duniani. Katika kupima huku ikadhihiri kuwa nusu ya kati ya dunia kwenye equator inazidi kuliko nusu ya poles kwa takriban kilomita 21.5. Yaani dunia imepungua katika ncha zake, yaani katika poles. Na inajuulikana maalumu kuwa sura ya dunia na masafa yake ndio msingi katika kuchorwa kwa ramani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika makafiri na baba zao walighurika na muhula waliopewa kwa kile walichokiona cha mali, watoto na maisha marefu, ndipo wakajikita kwenye ukafiri wao wasiepukane nao, na wakadhani kwamba wao hawataadhibiwa. Kwa kweli, wameghafilika na mpango uliopita, kwani Mwenyezi Mungu anaipunguza ardhi kwenye pembe zake kwa adhabu Anayoiteremsha kwa washirikina kila sehemu na kushindwa. Je, makafiri wa Makkah Wana nafasi ya kutoka nje ya uwezo wa Allah Mtukufu au kukataa kufa?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net