Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 29

Al-Anbiyaa 21:29

الأنبياء

وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّىٓ إِلَـٰهٌ مِّن دُونِهِۦ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Na yeyote kati yao atakayesema: "Hakika mimi ni mungu, badala yake", basi huyo tutamlipa Jahannamu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo madhalimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na yeyote kati yao atakaye sema: Mimi ni mungu, badala yake, basi huyo tutamlipa malipo yake Jahannamu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo wenye kudhulumu. [29]

[29] Na miongoni mwa Malaika atakaye sema: Mimi ni mungu wa kuabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, huyo tutamlipa kwa kumtia Jahannamu. Mfano wa malipo hayo tunamlipa kila mwenye kupindukia mipaka ya haki, na wakajidhulumu nafsi zao kwa kudai Ungu na kuingia katika ushirikina.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na yoyote miongoni mwa Malaika atakayedai kwamba yeye ni mungu pamoja na Allah Mtukufu, kwa kukadiria, basi malipo yake ni moto wa Jahanamu. Na mfano wa malipo hayo ndivyo tunavyomlipa kila dhalimu mshirikina.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net