Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 28

Al-Anbiyaa 21:28

الأنبياء

يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ٱرْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِۦ مُشْفِقُونَ

Maana

Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawamfanyii yeyote uombezi isipokuwa yule anayemridhia Yeye, nao kwa sababu ya kumhofu wanaogopa mno.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawamwombei yeyote ila yule anaye mridhia Yeye, nao kwa ajili ya kumwogopa wananyenyekea. [28]

[28] Mwenyezi Mungu anazijua hali zao zote na vitendo vyao vyote, walivyo vitanguliza na walivyo viakhirisha. Wala hawamwombei mtu kwake ila kwa aliye ridhia Mwenyezi Mungu. Na wao jinsi ya wingi wa khofu yao kumwogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumtukuza Yeye, daima wana hadhari naye..

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hakuna tendo lolote miongoni mwa matendo ya Malaika, lililopita au linalofuatia, isipokuwa Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, Analijua na anawahesabia kwalo. Na hawatangulii kumuombea yoyote isipokuwa yule ambaye Allah Mtukufu Ameridhika wamuombee. Na wao kwa kumuogopa Allah Mtukufu wanajizuiya kabisa kuenda kinyume na maamrisho Yake na makatazo Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net