Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 26

Al-Anbiyaa 21:26

الأنبياء

وَقَالُوا۟ ٱتَّخَذَ ٱلرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ۗ سُبْحَـٰنَهُۥ ۚ بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ

Maana

Na walisema: Arrahman (Mwingi wa rehema) alijifanyia mwana! Subhanahu (Ametakasika mbali na hayo!) Bali hao (wanaowaita wana) ni waja waliotukuzwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanasema: Arrahman, Mwingi wa Rehema, ana mwana! Subhanahu, Ametakasika na hayo! Bali hao (wanao waita wana) ni watumwa walio tukuzwa. [26]

[26] Na baadhi ya makafiri wa Kiarabu walisema: Arrahman, Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, ana mwana, kwa yale madai yao kuwa Malaika ni binti za Mwenyezi Mungu. Ametakasika na kuwa na mwana! Kwani hao Malaika ni waja wake walio tukuzwa tu kwa kuwakaribisha, na kwa wanavyo muabudu Yeye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na washirikina walisema, «Allah Mtukufu Amejifanyia mtoto» kwa madai yao kwamba Malaika ni watoto wa kike wa Allah Mtukufu. Ametakasika Allah Mtukufu na hilo! Malaika ni waja wa Allah Mtukufu waliokurubishwa waliohusishwa kwa kupewa matukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net