Al-Anbiyaa 21:25
الأنبياءوَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِىٓ إِلَيْهِ أَنَّهُۥ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱعْبُدُونِ
Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa tulimfunulia ya kwamba hakuna mungu isipokuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu. [25]
[25] Ewe Nabii! Sisi hatukumtuma Mtume yeyote kabla yako ila tulimpa wahyi (ufunuo) awafikishie watu wake kuwa hastahiki kuabudiwa isipo kuwa Mimi. Basi nisafieni ibada, iwe kwangu tu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hatukutuma kabla yako, ewe Mtume, mjumbe yoyote isipokuwa tunampatia wahyi kwamba hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah Mtukufu. Basi mtakasieni ibada Yeye Peke Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net