Al-Anbiyaa 21:23
الأنبياءلَا يُسْـَٔلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْـَٔلُونَ
Yeye haulizwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanaoulizwa kwa wayatendayo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yeye hahojiwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanao hojiwa kwa wayatendayo. [23]
[23] Yeye Subhanahu hahojiwi kwa anayo yatenda, kwani ni Yeye pekee mwenye utukufu na madaraka, Mwenye hikima na ujuzi. Hakosei katika kutenda chochote. Ni wao ndio watahisabiwa na kuhojiwa kwa wanayo yatenda, kwa kuwa wao hukosea kwa udhaifu wao na ujinga wao na kughilibiwa na matamanio.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Miongoni mwa dalili za kupwekeka Kwake, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kwa kuumba na kustahiki kuabudiwa ni kwamba Yeye Haulizwi kuhusu uamuzi Wake kwa viumbe Wake na kwamba viumbe Wake wote ndio wenye kuulizwa kuhusu matendo yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net