Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 22

Al-Anbiyaa 21:22

الأنبياء

لَوْ كَانَ فِيهِمَآ ءَالِهَةٌ إِلَّا ٱللَّهُ لَفَسَدَتَا ۚ فَسُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ رَبِّ ٱلْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ

Maana

Lau wangelikuwamo humo miungu wengine isipokuwa Mwenyezi Mungu, basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingeliharibika. Subhanallah (Ametakasika Mwenyezi Mungu), Bwana wa Kiti cha Enzi mbali na hayo wanayoyazua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lau wangeli kuwamo humo miungu wengine isipo kuwa Mwenyezi Mungu basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingeli fisidika. Subahana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu, Bwana wa A'rshi (Kiti cha Enzi), na hayo wanayo yazua. [22]

[22] Lau kuwa mbinguni na duniani kuna miungu isipo kuwa Mwenyezi Mungu wanao endesha mambo yao, basi ingeli haribika nidhamu iliyo simamishiwa hizo mbingu na ardhi kwa kuumbwa, na ikafikilia mwisho wa mpango na hikima. Basi na atakasike Mwenyezi Mungu, Mwenye Ufalme wote, na yote wanayo msingizia washirikina.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Lau mbinguni na ardhini kungekua na waungu wasiokuwa Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, wanaendesha mambo ya mbingu na ardhi, ungeharibika mpangilio wake. Basi Allah Mtukufu, Bwana wa ‛Arsh, Ametakasika na sifa za upungufu, na Ametakasika na kila sifa ambayo wakanushaji makafiri wanamsifu nayo ya urongo, uzushi na kila aibu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net