Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 109

Al-Anbiyaa 21:109

الأنبياء

فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَقُلْ ءَاذَنتُكُمْ عَلَىٰ سَوَآءٍ ۖ وَإِنْ أَدْرِىٓ أَقَرِيبٌ أَم بَعِيدٌ مَّا تُوعَدُونَ

Maana

Na kama wakigeuka, basi sema: Nimewatangazieni sawa sawa, wala sijui yako karibu au mbali hayo mliyoahidiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kama wakigeuka, basi sema: Nimekutangazieni sawa sawa, wala sijui yako karibu au mbali hayo mliyo ahidiwa. [109]

[109] Wakito ujali wito wako, basi waambie: Nimekufunzeni yote aliyo niamrisha Mola wangu Mlezi; na kwa hivyo tumekuwa sawa kwa kuyajua hayo. Wala mimi sijui hayo ya kufufuliwa na kuhisabiwa mliyo ahidiwa, yatakuwa karibu au mbali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi hawa wakiukengeuka uislamu waambie, «Ninawafikishia nyote kile ambacho Allah Mtukufu Aliyetukuka Amenitumia wahyi nacho. Mimi na nyinyi tuko sawa katika kuyajua yale ninayowaonya nayo na kuwatahadharisha, na mimi sijui, baada ya hapo, ni lini adhabu mliyoagiziwa itawashukia?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net