Al-Anbiyaa 21:108
الأنبياءقُلْ إِنَّمَا يُوحَىٰٓ إِلَىَّ أَنَّمَآ إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ
Sema: Hakika imefunuliwa kwangu ya kwamba hakika Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Je, Mmesilimu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Hakika imefunuliwa kwangu ya kwamba hakika Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Je! Mmesilimu?. [108]
[108] Ewe Nabii! Sema: Hakika kiini cha Wahyi aliyo nipa Mwenyezi Mungu ni kwamba hakika nyinyi hamna Mungu isipo kuwa Yeye. Na yote yaliyo bakia niliyo funuliwa yanafuata asili hii. Ikiwa mambo ni hivyo, basi inakuwajibikieni mjisalimishe na mnyenyekee kwa Mwenyezi Mungu peke yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, «Kile nilicholetewa wahyi na nikatumwa kwacho ni kwamba mola wenu Anayestahiki kuabudiwa, Peke Yake, ni Allah Mtukufu. Basi jisalimisheni Kwake na mnyoshe shingo zenu kwa kumuabudu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net