Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 104

Al-Anbiyaa 21:104

الأنبياء

يَوْمَ نَطْوِى ٱلسَّمَآءَ كَطَىِّ ٱلسِّجِلِّ لِلْكُتُبِ ۚ كَمَا بَدَأْنَآ أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُۥ ۚ وَعْدًا عَلَيْنَآ ۚ إِنَّا كُنَّا فَـٰعِلِينَ

Maana

Siku tutakapozikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi za vitabu. Kama tulivyoanza uumbaji wa mwanzo, tutaurudisha tena. Ni ahadi iliyo juu yetu. Hakika Sisi ni watendao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Siku tutakapo zikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi za vitabu. Kama tulivyo anza umbo la mwanzo tutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu yetu. Hakika Sisi ni watendao. [104]

[104] Siku tutapo zikunja mbingu kama zinavyo kunjwa karatasi katika kitabu. Na tutawarejeza viumbe kwa ajili ya hisabu na malipo. Wala hatushindwi kuwarejeza, kwani tuliwaumba mara ya kwanza. Na kama tulivyo waanza tutawarejeza. Ahadi yetu kwa hayo ni ahadi ya kweli. Daima Sisi tunatenda tunayo yaahidi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Siku ambayo tutaikunja mbingu kama vile ukurasa unaokunjiwa maandishi yaliyomo ndani, na tutawafufua viumbe kama vile walivyokuwa mwanzo walipozaliwa na mama zao. Hiyo ndiyo ahadi ya Allah Mtukufu isiyokwenda kinyume. Tumeliahidi hilo ahadi ya kweli tuliyojilazimisha nayo. Hakika sisi daima ni wenye kufanya tunaloahidi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net