Taa-Haa 20:115
طهوَلَقَدْ عَهِدْنَآ إِلَىٰٓ ءَادَمَ مِن قَبْلُ فَنَسِىَ وَلَمْ نَجِدْ لَهُۥ عَزْمًا
Na hapo zamani tuliagana na Adam, lakini alisahau, wala hatukupata kwake azimio kubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hapo zamani tuliagana na Adam, lakini alisahau, wala hatukuona kwake azma kubwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika tulimuusia Ãdam kabla hajakula kutoka kwenye ule mti, asile kutoka kwenye mti huo na tukamwambia kwamba Iblisi ni adui yako na mke wako, basi wasiwatoe nyinyi wawili kutoka Peponi, mkajasumbuka wewe na mke wako duniani. Basi Shetani akamshawishi, naye akamtii na akausahau wasia. Na hatukumpata na maazimio ya nguvu yenye kumfanya aitunze ile amri aliyopewa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net