Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 20 · Aya ya 114

Taa-Haa 20:114

طه

فَتَعَـٰلَى ٱللَّهُ ٱلْمَلِكُ ٱلْحَقُّ ۗ وَلَا تَعْجَلْ بِٱلْقُرْءَانِ مِن قَبْلِ أَن يُقْضَىٰٓ إِلَيْكَ وَحْيُهُۥ ۖ وَقُل رَّبِّ زِدْنِى عِلْمًا

Maana

Basi ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki. Wala usiifanyie haraka hii Qur-ani, kabla haujamalizika ufunuo wake. Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie elimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki. Wala usiifanyie haraka hii Qur'ani, kabla haujamalizika ufunuo wake. Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ametakasika Allah Mtukufu na kila upungufu, na Amekuwa juu, Aliye Mfalme Ambaye mamlaka Yake yamemtendesha nguvu kila mfalme na mjeuri, Mwenye kuendesha kila kitu, Ambaye Yeye Ndiye ukweli, na agizo Lake ni kweli, na onyo Lake ni kweli, na kila kitu kinachotoka Kwake ni kweli. Na usifanye haraka, ewe Mtume, ya kushindana na Jibrili katika kuipokea Qur’ani kabla hajaimaliza, na useme, «Mola wangu! Niongezee elimu juu ya ile uliyonifundisha».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Taa-Haa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net