Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 86

Al-Baqara 2:86

البقرة

أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشْتَرَوُا۟ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا بِٱلْـَٔاخِرَةِ ۖ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ ٱلْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ

Maana

Hao ndio walionunua uhai wa dunia kwa (uhai wa) Akhera. Kwa hivyo, hawatapunguziwa adhabu, wala hawatanusuriwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio walio nunua uhai wa dunia kwa (uhai wa) Akhera; kwa hivyo hawatapunguziwa adhabu wala hawatanusuriwa. [86]

[86] Na hayo ni kwa kuwa wamekhiari mapato ya hii dunia ipitayo kuliko neema za Akhera zitakazo dumu. Katika haya wamekuwa kama mtu aliye uza Akhera yake kwa ajili ya kununua dunia. Basi hawatapunguziwa adhabu ya Jahannam, wala hawatapata wa kuwaokoa nayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio waliofadhilisha uhai wa ulimwenguni juu ya Akhera, basi hawatapunguziwa adhabu wala wao hawatakuwa na msaidizi wa kuwanusuru na adhabu ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net