Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 70

Al-Baqara 2:70

البقرة

قَالُوا۟ ٱدْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِىَ إِنَّ ٱلْبَقَرَ تَشَـٰبَهَ عَلَيْنَا وَإِنَّآ إِن شَآءَ ٱللَّهُ لَمُهْتَدُونَ

Maana

Wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie ni yupi? Hakika tunaona ng'ombe wamefanana. Na kwa yakini, In sha Allah (Mwenyezi Mungu akipenda), tutaongoka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie ni yupi? Hakika tunaona ng'ombe wamefanana. Na kwa yakini, Inshaallah, Mwenyezi Mungu akipenda, tutaongoka. [70]

[70] Tena wakashikilia kuuliza kwao, wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie khasa huyo ni yupi? Kwani ng'ombe wanatudanganyikia sisi, hatujui. Na Inshallah, Mwenyezi Mungu akipenda, sisi tutaongokewa tumjue.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wana wa Isrãîl walimwambia Mûsã, “Tuombee Mola wako Atufafanulie sifa zake nyingine zisizokuwa zilizotangulia. Sababu ng’ombe wenye sifa hizi ni wengi. Kwa hivyo, tumechanganyikiwa hatujui tuchague yupi. Na sisi, Allah Mtukufu Anapotaka, tutaongokea kumjua ng’ombe ambaye ilitolewa amri achinjwe.”

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net