Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 69

Al-Baqara 2:69

البقرة

قَالُوا۟ ٱدْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا لَوْنُهَا ۚ قَالَ إِنَّهُۥ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ صَفْرَآءُ فَاقِعٌ لَّوْنُهَا تَسُرُّ ٱلنَّـٰظِرِينَ

Maana

Wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie ni ipi rangi yake? Akasema: Yeye anasema kuwa ng'ombe huyo ni wa manjano, na rangi yake imekoza, huwapendeza wanaomtazama.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Tuombee kwa Mola wako atupambanulie nini rangi yake? Akasema: Yeye anasema, kuwa Ng'ombe huyo ni wa manjano, na rangi yake imekoza, huwapendeza wanao mtazama. [69]

[69] Lakini walikakamia katika kutaradadi kwao, wakasema: Tutakie kwa Mola wako Mlezi atupambanulie nini rangi yake. Akawajibu: Mwenyezi Mungu anasema: Ng'ombe huyo ni wa rangi ya manjano iliyo koza, na safi. Ukimtazama anapendeza kwa usafi wa rangi yake ilivyo zagaa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakarudi kwenye kujadili kwao wakisema, “Mwambie Mola wako Atufafanulie rangi yake.” Akasema kuwaambia, “Yeye anasema kwamba huyo ni rangi ya manjano iliyoiva sana, anayemtia furaha mwenye kumwangalia.”

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net