Al-Baqara 2:62
البقرةإِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱلَّذِينَ هَادُوا۟ وَٱلنَّصَـٰرَىٰ وَٱلصَّـٰبِـِٔينَ مَنْ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَعَمِلَ صَـٰلِحًا فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ
Hakika Walioamini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema, basi watapata malipo yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa hofu juu yao, wala hawatahuzunika.[1]
[1] Hii ilikuwa hukumu yao kabla ya utume wa Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Na aya hii ilitajwa hapa kwa sababu Mwenyezi Mungu alipowakashifu wana wa Israili kwa dhambi zao, na maovu yao, huenda iliingia katika nafsi za baadhi yao kwamba sio wote waliyafanya hayo. Kwa hivyo, aya hii ikawaondoa wale ambao hawakuhusika katika kashfa hiyo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipwa yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika. [62]
[62] Wale walio amini, nao ni Manabii wa zamani, na Mayahudi, na Wakristo, na wanao tukuza nyota na malaika, na wanao uamini ujumbe wa Muhammad baada ya kuteuliwa kuwa ni Mtume, na wakaamini kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mmoja wa pekee, na wakaamini kuwa kupo kufufuliwa na kuhisabiwa Siku ya Kiyama, na wakatenda vitendo vyema duniani, basi watu hawa wana malipwa yao yaliyo wekewa kwa Mola wao Mlezi. Wala haitowapata khofu ya kuadhibiwa, na wala haitowafika huzuni kwa kukosa thawabu. Na Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa mwenye kutenda mema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Waumini wa ummah huu waliomuamini Allah Mtukufu na Mitume Wake na wakatekeleza Sheria Yake, na wale waliokuwa kabla ya kutumilizwa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, miongoni mwa ummah waliopita katika Mayahudi, Wanaswara na Wasabai (Sãbiũn), nao ni watu walioko kwenye tabia za maumbile na hawana dini maalumu wanayoifuata, wote hawa wakimuamini Allah Mtukufu, imani ya sawa iliyotakasika, wakaiamini Siku ya kufufuliwa na Malipo na wakafanya amali zenye kumridhi Allah Mtukufu, basi thawabu zao zimethibiti kwa Mola wao. Wao hawatakuwa na khofu juu ya mambo yao ya Akhera ambayo wao watayakabili. Na wala wao hawatahuzunika juu ya mambo ya dunia waliyoyakosa. Ama baada ya kutumilizwa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie yeye, kuwa ni mwisho wa Manabii na Mitume, kwa watu wote, Allah Mtukufu Hatakubali dini, kwa yoyote, isipokuwa ile aliyokuja nayo ambayo ni Uislamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net