Al-Baqara 2:57
البقرةوَظَلَّلْنَا عَلَيْكُمُ ٱلْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْكُمُ ٱلْمَنَّ وَٱلسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا۟ مِن طَيِّبَـٰتِ مَا رَزَقْنَـٰكُمْ ۖ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ
Na tukakutilieni kivuli kwa mawingu na tukakuteremshieni Manna na Salwa; tukakwambieni: 'Kuleni katika vitu vizuri hivi tulivyokuruzukuni.' Nao hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukakutilieni kivuli kwa mawingu na tukakuteremshieni Manna na Salwa; tukakwambieni: Kuleni vitu vizuri hivi tulivyo kuruzukuni. Nao hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wanajidhulumu nafsi zao. [57]
[57] Na katika fadhila zetu juu yenu ni kuwa tumekuleteeni mawingu yawe kama ni kivuli kukulindeni na mwako wa jua kali, na tukakuteremshieni Manna, nacho ni kitu kitamu kama asali kinaanguka juu ya miti linapo chomoza jua. Kadhaalika tumekuteremshieni Salwa, naye ni ndege aliye nona, nao wakikujieni kwa makundi asubuhi na jioni ili mle mstarehe. Na tukakwambieni: Kuleni vilivyo vyema katika riziki yetu. Hawa watu wakaikufuru neema. Na haya hayakutudhuru Sisi, lakini wamejidhulumu nafsi zao. Kwani madhara ya uasi unawarejea wao watendao. Katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na tukakuteremshieni Manna na Salwa" imetajwa kwa uhakika wa kisayansi, kwani hivi mwishoni imevumbuliwa kuwa madda za "Protein" zenye asli ya vinyama kama vile nyama na ndege ni bora kumfaa mtu kwa chakula kuliko "Protein" zinazotoka katika mimea na mboga. Na katika Manna mna sukari ya kumpa mtu nguvu na uchangamfu wa kufanyia kazi na kutaharaki huku na huku.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbukeni neema Zetu mlipokuwa mnahangaika kwenye ardhi, tukawaletea kiwingu cha kuwafinika ili kiwakinge na joto la jua, tukawateremshia mann, nacho ni kitu kifananacho na gundi chenye ladha ya asali; na tukawateremshia salwā, nayo ni aina ya ndege wafananao na tomboro; na tukawaambia, “Kuleni vitu vizuri tulivyowaruzuku na msiende kinyume n;a dini ya Allah Mtukufu,” lakini hamkufuata amri. Na wao hawakutudhulumu sisi kwa kuzikanusha neema hizi, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao, Kwani mwisho mbaya wa dhuluma utawarudia wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net