Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 56

Al-Baqara 2:56

البقرة

ثُمَّ بَعَثْنَـٰكُم مِّنۢ بَعْدِ مَوْتِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Maana

Kisha tukakufufueni baada ya kufa kwenu, ili mpate kushukuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukakufufueni baada ya kufa kwenu, ili mpate kushukuru. [56]

[56] Kisha tukakuzindueni kutokana na huko kudawaa kwenu na kupwelewa, na tukakufundisheni ili mpate kuishukuru neema yetu kwa hayo, na mpate kuiunga mkono Haki ya Mwenyezi Mungu kwa kupitia njia ya shukrani hii.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukawahuisha baada ya kufa kwenu kwa kimondo cha moto, ili muishukuru neema ya Allah Mtukufu kwenu. Kifo hiki kilikuwa ni adhabu kwao, kisha aliwafufua wakaendelea kuishi mpaka muda wao kumalizika.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net