Al-Baqara 2:46
البقرةٱلَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَـٰقُوا۟ رَبِّهِمْ وَأَنَّهُمْ إِلَيْهِ رَٰجِعُونَ
Ambao wana yakini kuwa hakika watakutana na Mola wao Mlezi na ya kuwa hakika ni wa kurejea kwake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ambao wana yakini kuwa hakika watakutana na Mola wao Mlezi na ya kuwa hakika watarejea kwake. [46]
[46] Hao ndio wanyenyekevu walio tulia nyoyo zao, ambao wanaiamini Siku ya mwisho, na wana yakini kuwa watakutana na Mola wao Mlezi wakati wa kufufuliwa, na kwake Yeye pekee ndio watarejea ili awahisabie kwa yale waliyo yatenda na awalipe kwayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wenye kumcha Allah Mtukufu na kutaraji Malipo yaliyoko Kwake, wenye kuamini kwa yakini kuwa wao ni wenye kukutana na Mola wao, Aliyetukuka na kushinda, baada ya kufa, na kuwa wao ni wenye kurejea Kwake Siku ya Kiama kwa kuhesabiwa na kulipwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net