Al-Baqara 2:45
البقرةوَٱسْتَعِينُوا۟ بِٱلصَّبْرِ وَٱلصَّلَوٰةِ ۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى ٱلْخَـٰشِعِينَ
Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu, [45]
[45] Na tafuteni msaada wa kutekeleza waajibu kwa subira na kuizuia nafsi isitende yanayo udhi. Katika hayo ni kwa kufunga Saumu, na kwa Swala ambalo ni jambo kubwa lenye kuusafisha moyo na kuzuia kutenda machafu na maovu, na kwa hivyo ndio yakawa mazito ila kwa wenye kupenda ut'iifu ambao nyoyo zao zimetulia kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Jisaidieni, katika mambo yenu, kwa subira za kila aina, na pia kwa Swala ambayo ni ngumu isipokuwa kwa wanyenyekevu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net