Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 265

Al-Baqara 2:265

البقرة

وَمَثَلُ ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَٰلَهُمُ ٱبْتِغَآءَ مَرْضَاتِ ٱللَّهِ وَتَثْبِيتًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ كَمَثَلِ جَنَّةٍۭ بِرَبْوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٌ فَـَٔاتَتْ أُكُلَهَا ضِعْفَيْنِ فَإِن لَّمْ يُصِبْهَا وَابِلٌ فَطَلٌّ ۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

Maana

Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kwa kuzitafuta radhi za Mwenyezi Mungu, na kuzipa nguvu roho zao ni kama mfano wa bustani iliyo mahali pa juu. Ikaifikia mvua kubwa na ikaleta mazao yake maradufu. Na hata kama haifikiwi na mvua kubwa, basi manyunyu tu yanatosha. Na Mwenyezi Mungu anayaona vyema mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mfano wa wale wanao toa mali zao kwa kuitafuta radhi ya Mwenyezi Mungu na kuzipa nguvu roho zao ni kama mfano wa bustani iliyo mahali pa juu, ikaifikia mvua kubwa na ikaleta mazao yake mardufu; na hata kama haifikiwi na mvua kubwa basi manyunyu hutosha. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda. [265]

[265] Hali ya wanao toa mali zao kwa kutaka kumridhi Mwenyezi Mungu na kuzithibitisha nafsi zao juu ya Imani, ni kama hali ya bustani, au kitalu, kwenye ardhi yenye rutuba iliyo nyanyuka (1) inayo faidika kwa maji mengi au kidogo. Ikija mvua kubwa huzaa mazao yake mardufu; na ikitopata mvua kubwa basi hata manyunyu kidogo hutosha kwa vile ardhi ni nzuri yenye kutoa mazao katika hali zote mbili. Basi Waumini wenye nyoyo safi hazipotei a'mali zao. Na vitendo vyenu havifichiki kwa Mwenyezi Mungu. (1) Neno la Qur'ani "ardhi iliyo nyanyuka" linaashiria yaliyo vumbuliwa na ilimu za sayansi za kisasa, kuwa maji ya chini yanakuwa yako mbali na mizizi. Kwa hivyo mizizi haiozi na vijizizi vidogo vinapata kunyonya chakula kwa wasaa na pia kuvuta pumzi. Kwa hivyo mazao yanakuwa mema, kwa mvua ijayo au hata manyunyu. (Nasi twajua mikarafuu au minazi ya bondeni haina maisha wala haistawi.)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mfano wa wale ambao wanatoa mali yao kwa kutaka radhi za Allah Mtukufu na kwa kuwa na itikadi iliyojikita ya kuwa ahadi ya Allah Mtukufu ni kweli, ni kama mfano wa bustani kubwa iliyoko kwenye ardhi ya juu iliyo nzuri iliyonyeshewa na mvua nyingi, yakaongezeka kwa wingi matunda yake. Na hata kama haingalinyeshewa na mvua nyingi, rasharasha la mvua lingalitosha kuifanya itoe ongezeko lingi la matunda. Basi hivyo ndivyo ulivyo utoaji wa watu wenye ikhlasi; amali zao zinakubaliwa mbele ya Allah Mtukufu na kuongezwa, ziwe ni chache au ni nyingi. Allah Mtukufu Ndiye Mwenye kuyaona ya nje na ya ndani, Anampa thawabu kila mtu kulingana na ikhlasi yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net