Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 21

Al-Baqara 2:21

البقرة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱعْبُدُوا۟ رَبَّكُمُ ٱلَّذِى خَلَقَكُمْ وَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

Maana

Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi aliyekuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu, ili mpate kucha (Mwenyezi Mungu).

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu, ili mpate kuokoka. [21]

[21] Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi aliye kuanzeni, akakuumbeni akakuleeni, kama alivyo waumba walio kutangulieni. Kwani Yeye ndiye Muumba wa kila kitu. Haya ni hivyo ili mpate kuzitayarisha nafsi zenu, na mzitengeneze kwa ajili ya utukufu wa Mwenyezi Mungu na uangalizi wake. Kwa hivyo nafsi zenu zitahirike na zipate kuifuata Haki, na ziogope mwisho muovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mwito utokao kwa Allah Mtukufu kwa binadamu wote: Muabuduni Allah Mtukufu Ambaye Amewalea kwa neema zake, na mumuogope wala msiende kinyume na dini Yake. Kwani yeye ndiye Aliyewaumba kutoka kwenye hali ya kutokuwako, na Akawaumba waliokuwa kabla yenu, ili muwe ni miongoni mwa wenye kumcha Allah Mtukufu ambao Yeye Ameridhika nao na wao wameridhika na Yeye.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net