Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 20

Al-Baqara 2:20

البقرة

يَكَادُ ٱلْبَرْقُ يَخْطَفُ أَبْصَـٰرَهُمْ ۖ كُلَّمَآ أَضَآءَ لَهُم مَّشَوْا۟ فِيهِ وَإِذَآ أَظْلَمَ عَلَيْهِمْ قَامُوا۟ ۚ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَذَهَبَ بِسَمْعِهِمْ وَأَبْصَـٰرِهِمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Maana

Unakaribia umeme huo kunyakua kuona kwao. Kila ukiwatolea mwangaza, wanatembea ndani yake. Na linapowawia giza, wanasimama. Na angelitaka Mwenyezi Mungu, angeliondoa kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza mno wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Unakaribia umeme kunyakua macho yao. Kila ukiwatolea mwangaza huenda, na unapo wafanyia giza husimama. Na angelitaka Mwenyezi Mungu angeliondoa kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. [20]

[20] Huu umeme mkali wa kuonya unakaribia kunyakua macho yao kwa ukali wake, nao kwa hakika unawamurikia njia kidogo ili wapate kwenda khatua chache kwa mwangaza wake, na unapo katika umeme kiza kinazidi, basi wao husimama hawajui watendeje, wamepotea. Basi hawa wanaafiki dalili na ishara zinapo watolea mwangaza huwa na hamu ya kutaka kuongoka, lakini mara punde hurejea kule kule kwenye ukafiri na unaafiki. Mwenyezi Mungu, Mkunjufu wa uwezo akitaka kitu hukitenda tu, haemewi na chochote katika ardhi wala katika mbingu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hizo pepe, kwa mng’aro wake, zinakaribia kuwatoa macho yao. Pamoja na hivyo, kila pepe ikiwang’arishia njia, wanatembea kwenye mwangaza wake, na ikiondoka, njia huwa na giza ikawabidi wasimame pale waliopo. Lau si Allah Mtukufu kuwapa muda, Angewaondolea masikizi yao ya kusikia na macho yao ya kuonea. Na Yeye ni mwenye uwezo wa kufanya hilo wakati wowote. Yeye ni Muweza wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net