Al-Baqara 2:194
البقرةٱلشَّهْرُ ٱلْحَرَامُ بِٱلشَّهْرِ ٱلْحَرَامِ وَٱلْحُرُمَـٰتُ قِصَاصٌ ۚ فَمَنِ ٱعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَٱعْتَدُوا۟ عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا ٱعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلْمُتَّقِينَ
Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Basi, anayewashambulia, nanyi mshambulieni kwa sawa na alivyowashambulia. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu kwa hakika yu pamoja na wacha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu. [194]
[194] Na pindi wakikushambulieni katika mwezi mtukufu msiache kupigana nao, kwani huo ni mtukufu kwao kama ulivyo kuwa mtukufu kwenu. Ikiwa wao watauvunja utukufu wake basi nanyi wakabilini kwa kuzilinda nafsi zenu katika huo mwezi. Na katika mambo matukufu na matakatifu pana sharia ya kisasi na kutendeana mfano kwa mfano. Anaye kushambulieni katika matakatifu yenu nanyi jilindeni na uadui huo kwa mfano wake. Na mcheni Mwenyezi Mungu, msikiuke mipaka katika kulipiza kisasi. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwanusuru wachamngu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kuwapiga kwenu vita, enyi Waumini, hao washirikina, katika mwezi ambao Allah Mtukufu Ameharamisha vita, ni malipo ya wao kuwapiga nyinyi vita mwezi mtukufu.Na yule anayekiuka yaliyoharamishwa na Allah Mtukufu ya pahali na zama, atapewa mateso yanayofanana na kitendo chake na yanayotokana na jinsi ya kosa alilolifanya. Basi atakayewafanyia uadui kwa vita au chinginecho, wapeni adhabu ifananayo na uovu wao, wala pasiwe na dhiki kwenu kuhusu hilo. kwa sababu wao ndio wenye kuanza uadui. Na muogopeni Allah Mtukufu na msipitishe kipimo cha kufanana kuadhibu. Na jueni kuwa Allah Mtukufu Yuko pamoja na wale wamchao na wanaomtii kwa kutekeleza Aliyoyafanya faradhi na kuyaepuka Aliyoyafanya haramu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net