Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 188

Al-Baqara 2:188

البقرة

وَلَا تَأْكُلُوٓا۟ أَمْوَٰلَكُم بَيْنَكُم بِٱلْبَـٰطِلِ وَتُدْلُوا۟ بِهَآ إِلَى ٱلْحُكَّامِ لِتَأْكُلُوا۟ فَرِيقًا مِّنْ أَمْوَٰلِ ٱلنَّاسِ بِٱلْإِثْمِ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

Maana

Wala msiliane mali zenu kwa batili, na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na hali mnajua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala msiliane mali zenu kwa baat'ili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na hali mnajua. [188]

[188] Mmekatazwa siku zote kula mali ya watu kwa njia isiyo ya haki. Mali ya mtu si halali kwenu ila kwa moja ya njia alizo wekea Sharia Mwenyezi Mungu, kama vile mirathi, au kutunukiwa kwa kupewa na mwenye mali, au kwa mkataba ulio sahihi wenye kuhalalisha kumiliki. Na huenda mmoja wenu hutafuta njia za kumpokonya mwenziwe haki ya mali yake kwa kupeleka kesi mahkamani ili yeye kwa kushirikiana na mahakimu au makadhi na kuleta ushahidi wa uwongo, au uwongo dhaahiri, au kutoa rushwa, wapate kula mali kwa dhulma. Huo ni uovu mno kwa wanao tenda, na malipo yao ni mabaya sana.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wasile baadhi yenu mali ya wengine kwa njia ya batili, kama kuapa yamini la urongo, kunyang’anya, kuiba, kuhonga, kula riba na mfano wa hayo.Wala msipeleke kwa mahakimu hoja potofu ili mpate kula kwa njia ya utesi mali ya kikundi cha watu wengine kwa njia ya batili, hali ya kuwa nyinyi mnajua uharamu wa hilo juu yenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net