Al-Baqara 2:186
البقرةوَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِى عَنِّى فَإِنِّى قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ ٱلدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا۟ لِى وَلْيُؤْمِنُوا۟ بِى لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ
Na waja wangu watakapokuuliza kunihusu Mimi, basi Mimi kwa hakika nipo karibu. Ninaitikia maombi ya mwombaji anaponiomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka. [186]
[186] Na Mimi nawajua vyema waja wangu, na najua wanayo yafanya na wanayo yawacha. Na Ewe Muhammad! Wakikuuliza waja wangu wakasema: Hivyo Mwenyezi Mungu yupo karibu nasi hata ajue tunayo yaficha na tunayo yatangaza na tunayo yawacha? Waambie: Mimi ni karibu nao zaidi kuliko wanavyo dhani. Na dalili ya hayo ni kuwa ombi la mwenye kuomba linafika wakati huo huo, na Mimi ndiye ninaye pokea hayo maombi wakati huo huo vile vile. Ilivyo kuwa Mimi nimewaitikia maombi yao basi na wao waniitikie Mimi kwa kuamini na kut'ii, kwani hiyo ndiyo njia ya kuongoka kwao na kusibu kwao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na watakapo kukuuliza, ewe Nabii, waja Wangu kuhusu Mimi, waambie, Mimi Niko karibu na wao, Nasikia maombi ya muombaji yoyote anaponiomba.Basi, wanitii Mimi katika Niliowaamrisha nayo na niliowakataza nayo na waniamini Mimi, wapate kuongokewa kwenye maslahi yao ya dini yao na dunia yao. Katika aya hii pana utoaji habari kutoka Kwa Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, kuhusu ukaribu Wake kwa waja Wake, ukaribu unaolingana na utukufu Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net