Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 171

Al-Baqara 2:171

البقرة

وَمَثَلُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ كَمَثَلِ ٱلَّذِى يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَآءً وَنِدَآءً ۚ صُمٌّۢ بُكْمٌ عُمْىٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ

Maana

Na mfano wa waliokufuru ni kama mfano wa anayempigia kelele asiyesikia isipokuwa wito na sauti tu. Ni viziwi, mabubu, vipofu, kwa hivyo hawaelewi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mfano wa walio kufuru ni kama mfano wa anaye mpigia kelele asiye sikia ila wito na sauti tu ni viziwi, mabubu, vipofu, kwa hivyo hawaelewi. [171]

[171] Na mfano wa kuwaita hao makafiri wanao pinga haki na uwongofu na wasiitikie wala wasifahamu wanaitiwa nini ni mfano wa mchunga kondoo anapo wasemeza hayawani. Hawafahamu kitu wala hawasikii ila sauti, wala hawaelewi kinginecho. Basi hao kadhaalika kwa mintarafu ya Haki ni viziwi wa kusikia, vipofu wa kuona, mabubu wa kusema. Hawatamki jema, wala hawatoi la akili.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na sifa za waliokufuru na wale walinganizi wao katika uongofu na imani ni kama sifa ya mchunga anayewapigia kelele wanyama na kuwakaripia, hali wao hawaelewi maana ya maneno yake isipokuwa wanasikia mwito na mlio wa sauti tu. Makafiri hao ni viziwi wameziba masikizi yao wasisikie haki, ni mabubu wamezifunga ndimi zao wasiitamke haki, ni vipofu macho yao hayazioni hoja za haki zilizo wazi. Kwa hivyo, wao hawatumii akili zao kwa mambo yenye kuwafaa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net