Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 105

Al-Baqara 2:105

البقرة

مَّا يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ وَلَا ٱلْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ ۗ وَٱللَّهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِۦ مَن يَشَآءُ ۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلْفَضْلِ ٱلْعَظِيمِ

Maana

Waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe heri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na Mwenyezi Mungu humteuwa amtakaye kumpa rehema yake. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walio kufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na Mwenyezi Mungu humkusudia kumpa rehema yake ampendaye. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa. [105]

[105] Na yafaa mjue kuwa hawa makafiri wa Kiyahudi na washirikina waabuduo masanamu hawakutakieni ila mdhurike tu, wala hawapendelei iteremke kheri yoyote kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na Mwenyezi Mungu hathamini chochote wanacho kipenda wala wanacho kichukia. Kwani Mwenyezi Mungu humteua amtakaye kwa kumkhusisha kumpa rehema yake, na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Makafiri, miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina, hawapendi mteremshiwe kheri, hata kama ni ndogo kabisa, itokayo kwa Mola wenu, iwe ni Qur’ani au elimu au ushindi au bishara njema. Allah Mtukufu Anamhusisha Amtakaye kwa rehema Zake za unabii na utume. Allah Mtukufu ni Mwenye fadhla nyingi zenye kuenea.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net