Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 94

Al-Kahf 18:94

الكهف

قَالُوا۟ يَـٰذَا ٱلْقَرْنَيْنِ إِنَّ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ فَهَلْ نَجْعَلُ لَكَ خَرْجًا عَلَىٰٓ أَن تَجْعَلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ سَدًّا

Maana

Wakasema: Ewe Dhul-Qarnain! Hakika Yaajuju na Maajuju wanafanya uharibifu katika ardhi. Basi je, tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Hakika Juju-wa-maajuju wanafanya uharibifu katika nchi. Basi je, tukulipe ujira ili utujengee baina yetu na wao ngome? [94]

[94] Walipo ziona nguvu zake na uwezo wake wakamtaka awasimamishie ngome ya kuwalinda na Juju-wa-maajuju. Nao hao ni watu wanao waonea maya, na wanawafisidia na kuwaharibia nchi yao. Na wao walikuwa watayari wamlipe ujira kwa kazi hiyo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakasema, «Ewe Dhulqarnain, kwa hakika, Ya’jûj na Ma’jûj – nao ni binadamu wa mataifa mawili makubwa- wanafanya uharibifu katika ardhi kwa kuangamiza mazao ya kilimo na vizazi, basi je, tukupatie ujira na tukukusanyie mali ili utuwekee kizuizi baina yetu na wao chenye kupambanua baina yetu na wao?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net