Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 93

Al-Kahf 18:93

الكهف

حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ بَيْنَ ٱلسَّدَّيْنِ وَجَدَ مِن دُونِهِمَا قَوْمًا لَّا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ قَوْلًا

Maana

Hata alipofika katikati ya milima miwili, alikuta nyuma yake kaumu ambao walikaribia kutofahamu neno lolote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hata alipo fika baina ya milima miwili, alikuta nyuma yake watu ambao takriban hawakuwa wanafahamu lolote. [93]

[93] Mpaka akafika - katika safari yake ya tatu - pahala mbali baina ya milima miwili mirefu...Na huko akakuta watu ambao hawafahamu wanalo ambiwa ila kwa uzito na mashaka. Hiyo ngome au boma baina ya milima miwili iliyo tajwa katika maelezo ya juu ni milima ya Azarbajan na Arminia, na kauli nyingine ni kaskazini ya mwisho katika jimbo la Turkistan.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mpaka alipofika baina ya majabali mawili yaliyozuia vilivyo nyuma yake, aliwakuta hapo watu wasiokaribia kuelewa maneno ya wasiokuwa wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net