Al-Kahf 18:9
الكهفأَمْ حَسِبْتَ أَنَّ أَصْحَـٰبَ ٱلْكَهْفِ وَٱلرَّقِيمِ كَانُوا۟ مِنْ ءَايَـٰتِنَا عَجَبًا
Kwani unadhani ya kwamba wale watu wa Pangoni na Maandishi ndio walikuwa tu ajabu miongoni mwa ishara zetu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Bali unadhani ya kwamba wale Watu wa Pangoni na Maandishi walikuwa ni ajabu miongoni mwa ishara zetu? [9]
[9] Walio pumbazwa na starehe za dunia wanakanya kufufuliwa, ilihali hakika ya mambo inathibitisha pana uhai baada ya usingizi mrefu. Na hichi kisa cha Watu wa Pangoni kwenye mlima na bao lilio andikwa majina yao baada ya kufa kwao hakikuwa ni ajabu ya pekee, tukaziacha ishara zote nyenginezo. Ijapo kuwa kisa hicho si cha kawaida, lakini hakikuwa ndio cha ajabu kushinda ishara zetu nyengine zenya kuonyesha uweza wetu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Usidhani kwamba kisa cha watu wa pangoni (asḥãb al-kahf) na ubao ulioandikwa majina yao ni jambo geni la ajabu miongoni mwa alama zetu. Kuumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ni jambo la ajabu zaidi kuliko hilo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net