Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 10

Al-Kahf 18:10

الكهف

إِذْ أَوَى ٱلْفِتْيَةُ إِلَى ٱلْكَهْفِ فَقَالُوا۟ رَبَّنَآ ءَاتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا

Maana

Vijana hao walipokimbilia kwenye pango, na wakasema, "Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uongofu katika jambo letu."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Vijana hao walipo kimbilia kwenye pango walisema: Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uwongofu katika jambo letu. [10]

[10] Taja pale walipo kwenda hao vijana kwenye pango, wakafanya hapo ndipo pahali pa kujificha baada ya kukimbia ushirikina na washirikina kuhifadhi Dini yao. Wakasema: Ewe Mola wetu Mlezi! Tupe maghfira kutoka kwako, na utulinde na adui yetu, na tusahilishie hidaya na tawfiki katika mambo yetu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kumbuka, ewe Mtume, pindi walipohamia vijana Waumini kwenye pango kwa kuchelea wasiteswe na watu wao na kulazimishwa kuabudu masanamu, na wakasema, «Mola wetu! Tupe rehema kutoka kwako, ambayo kwayo ututhibitishe na utuhifadhi na shari, na utusahilishie njia ya sawa yenye kutupelekea kufanya matendo unayoyapenda, tuwe waongofu na tusiwe wapotevu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net