Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 83

Al-Kahf 18:83

الكهف

وَيَسْـَٔلُونَكَ عَن ذِى ٱلْقَرْنَيْنِ ۖ قُلْ سَأَتْلُوا۟ عَلَيْكُم مِّنْهُ ذِكْرًا

Maana

Na wanakuuliza kuhusu Dhul-Qarnain. Waambie: nitawasomea baadhi ya hadithi yake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake. [83]

[83] Ewe Mtume! Baadhi ya makafiri wanakuuliza khabari za Dhul-Qarnaini. Waambie nitakusimulieni baadhi ya khabari zake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hawa washirikina wa watu wako wanakuuliza, ewe Mtume, kuhusu habari ya Dhulqarnain, mfalme aliye mwema, waambie, «Nitawapa habari kuhusu yeye ya kuwaachia kumbukumbu mpate kuikumbuka na kuizingatia».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net