Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 82

Al-Kahf 18:82

الكهف

وَأَمَّا ٱلْجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَـٰمَيْنِ يَتِيمَيْنِ فِى ٱلْمَدِينَةِ وَكَانَ تَحْتَهُۥ كَنزٌ لَّهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَـٰلِحًا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَن يَبْلُغَآ أَشُدَّهُمَا وَيَسْتَخْرِجَا كَنزَهُمَا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ وَمَا فَعَلْتُهُۥ عَنْ أَمْرِى ۚ ذَٰلِكَ تَأْوِيلُ مَا لَمْ تَسْطِع عَّلَيْهِ صَبْرًا

Maana

Na ama ukuta ule, huo ulikuwa ni wa vijana wawili mayatima kule mjini. Na chini yake ilikuwapo hazina yao; na baba yao alikuwa ni mtu mwema. Basi Mola wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima wao na wajitolee hazina yao wenyewe, hii ikiwa ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Wala mimi sikutenda hayo kwa amri yangu. Hiyo ndiyo tafsiri ya hayo ambayo wewe hukuweza kuyasubiria.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ama ukuta, huo ulikuwa ni wa vijana wawili mayatima kule mjini. Na chini yake ilikuwako khazina yao; na baba yao alikuwa ni mtu mwema. Basi Mola wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima na wajitolee khazina yao wenyewe, kuwa ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Wala mimi sikutenda hayo kwa amri yangu. Hiyo ndiyo tafsiri ya hayo ambayo wewe hukuweza kuyasubiria. [82]

[82] Ama ule ukuta nilio usimamisha, bila ya ujira, ulikuwa wa vijana wawili mayatima katika watu wa ule mji. Na chini yake ilikuwako khazina walio achiwa na baba yao. Naye alikuwa ni mtu mwema. Basi Mwenyezi Mungu alitaka kuwahifadhia khazina yao ile mpaka wakue wawe na akili zao, na wajitolee wenyewe khazina yao kuwa ni rehema kwao, na kumtukuza baba yao kwa kupitia dhuriya zake. Nami sikufanya niliyo yafanya kwa jitahada ya nafsi yangu. Bali nimefanya hayo kwa kuongozwa na Mwenyezi Mungu. Hii ni tafsiri ya hayo yaliyo fichikana kwako wewe Musa, nawe usiweze kuyavumilia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ama ukuta niliyoutengeneza, baada ya kuwa umeinama, mpaka ukawa sawa, ulikuwa ni wa wavulana wawili mayatima hapo kijijini, na chini yake kulikuwa na hazina yao ya dhahabu na fedha, na baba yao alikuwa mtu mwema, Mola wako Akataka wawe wakubwa, wapate nguvu na waitoe hazina yao kwa rehema itokayo kwa Mola wako. Na mimi sikuyafanya yote haya, ewe Mûsã, kwa amri yangu, kwa hakika nimeyafanya kwa amri ya Allah Mtukufu. Hayo niliyokueleza sababu zake ndiyo mwisho wa mambo ambayo hukuweza kuyavumilia kwa kuacha kuyauliza na kunipinga kwayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net