Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 24

Al-Kahf 18:24

الكهف

إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ ۚ وَٱذْكُر رَّبَّكَ إِذَا نَسِيتَ وَقُلْ عَسَىٰٓ أَن يَهْدِيَنِ رَبِّى لِأَقْرَبَ مِنْ هَـٰذَا رَشَدًا

Maana

Isipokuwa Mwenyezi Mungu akipenda. Na mkumbuke Mola wako Mlezi pale unaposahau, na sema: huenda Mola wangu Mlezi ataniongoa kwenye uongozi ulio karibu zaidi kuliko huu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Isipo kuwa Mwenyezi Mungu akipenda. Na mkumbuke Mola wako Mlezi pale unapo sahau, na sema: Asaa Mola wangu Mlezi ataniongoa kwenye uwongozi ulio karibu zaidi kuliko huu. [24]

[24] Ila kusema huko kuambatane na kupenda kwa Mwenyezi Mungu kwa kusema: Inshallah, yaani Mwenyezi Mungu akipenda. Na ukisahau jambo, basi kimbilia kumtaja Mwenyezi Mungu; na useme unapo azimia kufanya jambo na kuliambatanisha na kupenda kwa Mwenyezi Mungu: Huenda Mola wangu Mlezi akaniwafikisha kwenye bora kuliko nililo azimia kufanya, na lenye kuongoka zaidi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Isipokuwa ufungamanishe neno lako na matakwa ya Allah Mtukufu na useme, «Allah Mtukufu Atakapo.» Na mkumbuke Mola wako unaposahau kwa kusema, «Allah Mtukufu Atakapo.» Na kila unaposahau, mtaje Allah Mtukufu, kwani kumtaja Allah Mtukufu huondosha kusahau, na useme, «Matarajio ni kwamba Mola wangu Aniongoze njia ya karibu zaidi yenye kufikisha kwenye uongofu na ya sawa».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net