Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 91

Al-Israa 17:91

الإسراء

أَوْ تَكُونَ لَكَ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَعِنَبٍ فَتُفَجِّرَ ٱلْأَنْهَـٰرَ خِلَـٰلَهَا تَفْجِيرًا

Maana

Au uwe na bustani ya mitende na mizabibu, na utupitishie mito kati yake ikimiminika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au uwe na kitalu cha mitende na mizabibu, na utupitishie mito kati yake ikimiminika. [91]

[91] Au uwe nacho kitalu Makka cha mitende na mizabibu chenye kupita mito kati yake! (Kwa kujua kuwa ardhi ya Makka ni kavu haioti kitu.)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

«Au uwe na shamba lenye aina za mitende na mizabibu, na uifanye mito ni yenye kupita kati yake kwa wingi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net