Al-Israa 17:90
الإسراءوَقَالُوا۟ لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ تَفْجُرَ لَنَا مِنَ ٱلْأَرْضِ يَنۢبُوعًا
Na walisema, "Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemichemi katika ardhi hii.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walisema: Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchem katika ardhi hii. [90]
[90] Ilipo dhihiri kushindwa kwao na Qur'ani, na wakabanwa kwa hoja, wakataka waletewe ishara nyingine na miujiza mingine. Hicho ni kitendo cha mwenye kushindwa hoja, aliye emewa na kutahayari. Ndio wakasema: Hatutokuamini mpaka ututimbulie katika ardhi ya Makka chemchem ambayo maji yake hayakatiki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Qur’ani ilipowaelemea washirikina na ikawashinda, walitaka miujiza kulingana na mapendekezo yao wakasema, «Hatutakuamini, ewe Muhammad, na hatutafanya vile unavyosema mpaka utupasulie kwenye ardhi ya Makkah chemchemi ya maji yenye kupita».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net