Al-Israa 17:47
الإسراءنَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَسْتَمِعُونَ بِهِۦٓ إِذْ يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ وَإِذْ هُمْ نَجْوَىٰٓ إِذْ يَقُولُ ٱلظَّـٰلِمُونَ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا رَجُلًا مَّسْحُورًا
Sisi tunajua vyema kabisa sababu wanayosikilizia wanapokusikiliza, na wanaponong'ona. Wanaposema hao madhalimu: Nyinyi hamumfuati isipokuwa mwanamume aliyerogwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sisi tunajua vyema kabisa sababu wanayo sikilizia wanapo kusikiliza, na wanapo nong'ona. Wanapo sema hao madhaalimu: Nyinyi hamumfuati isipo kuwa mtu aliye rogwa. [47]
[47] Sisi tunajua vyema vile wanavyo isikiliza Qur'ani nao ilhali wanaikejeli na kuifanyia maskhara na huku wanakusikiliza. Nao wanayaficha yaliyo semwa. Na hiyo ndiyo kauli ya wenye kudhulumu katika siri zao, wakisema: Ikiwa mtamfuata huyu basi hamumfuati ila mtu aliye geuzwa akili yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sisi tunayajua zaidi yale wanayoyasikiliza viongozi wa Kikureshi pale wakusikilizapo na hali nia zao ni mbovu. Kusikiliza kwao si kwa ajili ya kutaka kuogoka na kuikubali haki. Na sisi tunajua kule kunong’onezana kwao wanaposema, «Hamumfuati isipokuwa ni mwanamume aliyerogwa na akili yake ikabadilika».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net