Al-Israa 17:46
الإسراءوَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِىٓ ءَاذَانِهِمْ وَقْرًا ۚ وَإِذَا ذَكَرْتَ رَبَّكَ فِى ٱلْقُرْءَانِ وَحْدَهُۥ وَلَّوْا۟ عَلَىٰٓ أَدْبَـٰرِهِمْ نُفُورًا
Na tunaweka vifuniko juu ya nyoyo zao wasije wakaifahamu, na tunaweka kwenye masikio yao uziwi. Na unapomtaja katika Qur-ani Mola wako Mlezi peke yake, basi wao hugeuka nyuma wakaenda zao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tunaweka vifuniko juu ya nyoyo zao wasije wakaifahamu, na tunaweka kwenye masikio yao uziwi. Na unapo mtaja katika Qur'ani Mola wako Mlezi peke yake, basi wao hugeuka nyuma wakenda zao. [46]
[46] Na kwa mujibu wa hikima yetu ya kupotoa na kuongoa huweka vifuniko juu ya nyoyo zao, wasipate kuifahamu Qur'ani ilivyo. Na katika masikio yao hutia uziwi basi hawasikii lenye manufaa kwao. Hayo ni kwa sababu ya kupindukia katika inda yao na majivuno yao. Na pale unapo mtaja Mola wako Mlezi katika Qur'ani peke yake bila ya kuwataja miungu yao, wao basi hurejea nyuma wakaacha kukusikiliza.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tumeweka juu ya nyoyo za washirikina vifuniko, wasipate kuifahamu Qur’ani, na tumejaalia uziwi ndani ya masikio yao, wasipate kuisikia. Na umtajapo Mola wako katika Qur’ani uwalinganiapo kwenye kumpwekesha Yeye na ukatazapo kushirikishwa, wao hurudi kinyumenyume kwa kuyakimbia maneno yako, kwa kufanya kiburi na kujiona kuwa ni wakubwa mno wa kutofaa kumpwekesha Allah Mtukufu, Peke Yake, katika kumuabudu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net