Al-Israa 17:37
الإسراءوَلَا تَمْشِ فِى ٱلْأَرْضِ مَرَحًا ۖ إِنَّكَ لَن تَخْرِقَ ٱلْأَرْضَ وَلَن تَبْلُغَ ٱلْجِبَالَ طُولًا
Wala usitembee katika ardhi kwa kiburi. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi na kamwe huwezi kufikia urefu wa milima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala kufikia urefu wa milima. [37]
[37] Wala usitembee katika ardhi kwa kiburi na majivuno. Kwani vyovyote utavyo fanya huwezi kuipasua ardhi kwa nguvu za mkanyago wako, na kama utavyo kuwa mrefu huwezi kuipita urefu milima.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na usitembee ardhini kwa kujigamba na kujivuna, kwani wewe hutaipasua ardhi kwa kutembea juu yake kwa namna hiyo na hutaifikia milima katika urefu kwa kujigamba kwako, kujivuna kwako na kutakabari kwako.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net