Al-Israa 17:36
الإسراءوَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِۦ عِلْمٌ ۚ إِنَّ ٱلسَّمْعَ وَٱلْبَصَرَ وَٱلْفُؤَادَ كُلُّ أُو۟لَـٰٓئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْـُٔولًا
Wala usiyafuate usiyo na elimu nayo. Hakika kusikia, na kuona, na (ufahamu wa) moyo hivyo vyote itaulizwa juu yake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa. [36]
[36] Ewe mtu! Usifuate maneno wala vitendo usivyo vijua. Basi usiseme: Nimesikia...na hali hukusikia. Au: Najua...na hali hujui. Kwani masikio, macho na moyo, vyote hivyo Siku ya Kiyama vitamuuliza mtu kwa alivyo tenda kwavyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na usiyafuate, ewe binadamu, usiyoyajua, lakini hakikisha na uthibitishe. Hakika ya binadamu ni mwenye kuulizwa juu ya yale ambayo alitumia masikio yake, macho yake na moyo wake kuyafikia. Basi akivitumia vitu hivyo katika wema atapata malipo mema na akivitumia katika uovu atapata mateso.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net