Al-Israa 17:34
الإسراءوَلَا تَقْرَبُوا۟ مَالَ ٱلْيَتِيمِ إِلَّا بِٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُۥ ۚ وَأَوْفُوا۟ بِٱلْعَهْدِ ۖ إِنَّ ٱلْعَهْدَ كَانَ مَسْـُٔولًا
Wala msiyakaribie mali ya yatima, isipokuwa kwa njia iliyo nzuri zaidi, mpaka afike utu uzimani. Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itaulizwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala msiyakaribie mali ya yatima, isipo kuwa kwa njia iliyo bora, mpaka afike utuuzimani. Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa. [34]
[34] Wala msiyatumie mali ya yatima ila kwa njia iliyo bora kabisa, ya kuiamirisha na kuikuza. Na endeleeni hivyo mpaka huyo mtoto afike umri wa utambuzi kuweza kuendesha mambo yake. Na akisha fika hivyo basi mkabidhini mali yake, na timizeni ahadi zote mlizo chukua. Kwani Mwenyezi Mungu atamsaili (atamuliza) aliye vunja ahadi kwa kuvunja kwake, na atamhisabia kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wala msitumie mali ya watoto waliofiliwa na wazazi wao nao wako chini ya miaka ya kubaleghe na wakawa wako chini ya usimamizi wenu, isipokuwa kwa njia ambayo ni nzuri kwao, nayo ni kuizalisha na kuikuza, mpaka afikie mtoto yatima miaka ya kubaleghe na utumiaji mzuri wa mali. Na timizeni utekelezaji wa kila ahadi mliyojilazimisha nayo, kwani Allah Mtukufu Atamuuliza mwenye kuweka ahadi kuhusu hiyo ahadi Siku ya Kiyama, Atamlipa akiitimiza na kuitekeleza na Atamuadhibu akienda kinyume nayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net