Al-Israa 17:33
الإسراءوَلَا تَقْتُلُوا۟ ٱلنَّفْسَ ٱلَّتِى حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلْحَقِّ ۗ وَمَن قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِۦ سُلْطَـٰنًا فَلَا يُسْرِف فِّى ٱلْقَتْلِ ۖ إِنَّهُۥ كَانَ مَنصُورًا
Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipokuwa kwa haki. Na aliyeuliwa kwa kudhulumiwa, basi hakika tumempa msimamizi wake mamlaka. Lakini asipitilize kiasi katika kuua. Kwani yeye anasaidiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa. [33]
[33] Wala msiuwe nafsi yoyote ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa ila kuuwa huko kukiwa kwa haki, kwa kuwa nafsi hiyo inastahiki kuuwawa kwa ajili ya kisasi au kuwa ni adhabu ya sharia. Na mwenye kuuliwa kwa kudhulumiwa Sisi tumempa jamaa yake wa karibu haki juu ya yule muuwaji, kwa kutaka kwa Qadhi auliwe kwa kisasi. Lakini naye asipite mpaka katika kuuwa, akataka kumuuwa mtu mwengine asiye kuwa muuwaji, au kwa kuwauwa wawili badala ya mmoja. Kwani Mwenyezi Mungu amemsaidia huyo kwa kumpa haki ya kisasi au kulipwa fidiya. Basi haimfalii kukiuka mipaka iliyo wekwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wala msiiue nafsi ambayo Allah Mtukufu Ameharamisha kuuawa, isipokuwa kwa haki ya kisheria, kama kisasi au kumpiga mawe mzinifu aliyeingia kwenye hifadhi ya ndoa au kumuua aliyeritadi. Na mwenye kuuawa pasi na haki ya kisheria, basi tumempa msimamizi wa mambo yake, awe ni mrithi au ni hakimu, uwezo wa kutaka muuaji auawe au kutaka dia. Na haifai kwa msimamizi wa mambo ya aliouawa kupita mpaka wa Allah Mtukufu katika kuchukua kisasi, kama vile kuua watu wawili au wengi kwa mmoja au kumuuwa muuaji kwa njia ya kumtesa. Allah Mtukufu ni Mwenye kumsaidia msimamizi wa aliyeuawa juu ya aliyeua mpaka aweze kumuua kwa njia ya kisasi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net