Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 14 · Aya ya 44

Ibrahim 14:44

ابراهيم

وَأَنذِرِ ٱلنَّاسَ يَوْمَ يَأْتِيهِمُ ٱلْعَذَابُ فَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ رَبَّنَآ أَخِّرْنَآ إِلَىٰٓ أَجَلٍ قَرِيبٍ نُّجِبْ دَعْوَتَكَ وَنَتَّبِعِ ٱلرُّسُلَ ۗ أَوَلَمْ تَكُونُوٓا۟ أَقْسَمْتُم مِّن قَبْلُ مَا لَكُم مِّن زَوَالٍ

Maana

Na waonye watu siku itakapowajia adhabu, na wale waliodhulumu waseme, "Ewe Mola wetu Mlezi! Tuahirishe muda kidogo tuitikie wito wako na tuwafuate Mitume." Kwani nyinyi hamkuapa zamani kwamba kamwe hamuwezi kuondoka?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na waonye watu siku itapo wajia adhabu, na walio dhulumu waseme: Ewe Mola wetu Mlezi! Tuakhirishe muda kidogo tuitikie wito wako na tuwafuate Mitume. Kwani nyinyi si mliapa zamani kwamba hamtaondokewa? [44]

[44] Ewe Nabii! Waeleze watu khabari za vitisho vya Siku ya Kiyama watapo sema walio zidhulumu nafsi zao kwa ukafiri na maasi: Mola wetu Mlezi, tuakhirishie adhabu, uturejeshe duniani, na utupe muhula kwa muda mdogo, walau tudiriki kuitikia wito wako wa Tawhidi na kuwafuata Mitume. Nao wataambiwa: Leo ndio mwasema haya? Na mmesahau ya kwamba mliapa nyinyi ya kuwa mkifa neema hizi hazitokuondokeeni mtapo fufuliwa Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na waonye, ewe Mtume, wale watu ambao wewe umetumilizwa kwao, adhabu ya Allah Mtukufu Siku ya Kiyama. Na hapo wale waliojidhulumu kwa kukanusha watasema, «Ewe Mola,wetu! Tupe muhula wa muda mchache, tutakuamini na tutawasadiki Mitume wako.» Na wataambiwa kwa kuchezwa shere, «Je, hamkuapa katika uhai wenu kwamba hamtaondoka ulimwenguni kwenda Akhera, na msiamini kufufuliwa huku?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ibrahim

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net