Ibrahim 14:43
ابراهيممُهْطِعِينَ مُقْنِعِى رُءُوسِهِمْ لَا يَرْتَدُّ إِلَيْهِمْ طَرْفُهُمْ ۖ وَأَفْـِٔدَتُهُمْ هَوَآءٌ
Watakuwa mbioni, vichwa juu, huku macho yao hayapepesi, na nyoyo zao zitakuwa tupu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nao wako mbioni, vichwa juu, na macho hayapepesi, na nyoyo zao tupu. [43]
[43] Nao wako mbioni kumwendea anaye wita, vichwa vyao vimeelekea juu mbinguni, macho yao hayapepesi hata wakitaka, na nyoyo zao tupu hazina wazo lolote kwa wingi wa khofu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Siku watakayosimama madhalimu kutoka makaburini mwao wakikimbilia kumwitika mlinganizi wakiinua vichwa vyao, hawaoni chochote kwa kitisho cha kisimamo, na hali nyoyo zao ni tupu hazina kitu ndani yake, kwa hofu kubwa na kuogopa kitisho cha wanayoyaona.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net