Ibrahim 14:34
ابراهيموَءَاتَىٰكُم مِّن كُلِّ مَا سَأَلْتُمُوهُ ۚ وَإِن تَعُدُّوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ لَا تُحْصُوهَآ ۗ إِنَّ ٱلْإِنسَـٰنَ لَظَلُومٌ كَفَّارٌ
Na akawapa katika kila mlichomuomba. Na mkihesabu neema za Mwenyezi Mungu, hamuwezi kuzidhibiti. Hakika mwanadamu ni dhalimu mkubwa, mwenye kukufuru sana neema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na akakupeni kila mlicho muomba. Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamwezi kuzidhibiti. Hakika mwanaadamu ni dhaalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema. [34]
[34] Na akakutengenezeeni yote mnayo yahitajia katika maisha yenu ambayo anastahiki kuombwa, sawa sawa ikiwa mmemuomba au la. Na mkizihisabu neema alizo kuneemesheni Mwenyezi Mungu, hamwezi kuzidhibiti namna zake, seuze idadi yake! Hakika huyo mwenye kukanya ambaye akalipa ukafiri kuwa ni malipo ya neema alizo pewa, basi ni mwingi wa udhalimu na ukafiri!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Akawapa nyinyi kila mlichomuomba. Na mkihesabu ili kujua idadi ya neema za Allah Mtukufu juu yenu, hamtaweza kuzihesabu na kudhibiti idadi yake wala kusimama itakikanavyo kushukuru kwa hizo kwa wingi wake na aina zake. Hakika Binadamu ni mwingi wa kujidhulumu nafsi yake, ni mwingi wa kukanusha neema za Mola wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net